👉 Mradi huo ambao utekelezaji wake unatarajia kuanzia mapema mwezi Agosti 2025, utahusisha ukarabati mkubwa wa Meli ya MV Songea
DAR ES SALAAM. KAMPUNI Ya Meli Tanzania ( TASHICO) imepanga kutumia kiasi cha Shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kimkakati wa kuboresha huduma za usafiri wa Meli katika Ziwa Nyasa.
Mradi huo ambao utekelezaji wake unatarajia kuanzia mapema mwezi Agosti 2025, utahusisha ukarabati mkubwa wa Meli ya MV Songea,"
Ikiwa na uwezo wa kubeba angalau abiria 212, Meli ya MV Songea ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka Kiwira kwenda Mbaba Bay ilisitisha huduma zake tangu mwaka 2017 kwa sababu ya uchakavu, hali iliyosababisha kudorora kwa huduma ya usafiri katika Ziwa hilo maarufu lilopo Kusini-Magharibi mwa Tanzania.
Akiongea na 'Swahili News' katika mahojiano maalumu, Mkurugenzi Mkuu wa TASHICO, Bwn. Eric Hamissi amesema Kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 4 Ili kuhakikisha Meli hiyo muhimu inarudi majini.
Amesema, tangu mwaka 2017 wakati ambapo MV Songea ilisimamisha huduma, abiria wanaotumia usafiri wa njia ya maji katika Ziwa Nyasa walikuwa wakihudumiwa na Meli Moja tu, MV Mbeya II.
Mkurugenzi Hamissi aliongeza kuwa, kwa sasa TASHICO inatekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuongeza tija na upatikanaji mkubwa wa huduma za Meli katika Maziwa yote Makuu nchini Tanzania.
Kwa mfano, amesema, Kampuni imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 171 katika mwaka wa fedha 2025/26 ili kusaidia kukamilisha miradi mbalimbali ambayo ilianza wakati wa mwaka wa fedha uliopita.
" Tunamshukuru sana Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akiwezesha Kampuni ya Meli Tanzania kupata bejeti nzuri inayowezesha ufanisi mkubwa katika kukamilisha miradi ya kimkakati ya kuinua huduma ya usafiri katika Maziwa Makuu," Alishukuru
Post a Comment