KAMPUNI YA HQ TANZANIA YATOA VIFAA TIBA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU SBHD FOUNDATION




MUHTASARI 

Vifaa hivyo vitasaidia kuimarisha huduma zinazotolewa kwa watoto hao na kuchangia katika juhudi za kuwawezesha kuishi kwa kujitegemea zaidi.


DAR ES SALAAM: KAMPUNI ya HQ Tanzania imetoa msaada wa vifaa tiba kwa watoto wenye ulemavu wanaolelewa na Kituo cha SBHD Foundation, hatua inayolenga kusaidia ustawi na kuboresha maisha ya watoto wenye mahitaji maalum.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi wa SBHD Foundation, Bi. Suma Geofrey, alisema vifaa hivyo vitasaidia kuimarisha huduma zinazotolewa kwa watoto hao na kuchangia katika juhudi za kuwawezesha kuishi kwa kujitegemea zaidi.



Aidha, alitoa shukrani kwa uongozi wa HQ Tanzania kwa mchango huo, ambapo amesema ushirikiano kati ya sekta binafsi na taasisi zinazohudumia makundi maalum una nafasi muhimu katika kuimarisha ustawi wa jamii.

Bi. Suma pia alitoa wito kwa wadau mbalimbali na wananchi kuendelea kushiriki katika kusaidia watoto wenye mahitaji maalum kupitia michango na huduma mbalimbali zinazoweza kuboresha mazingira yao ya maisha na kujifunzia.




Post a Comment

Previous Post Next Post